NATIONAL PARKS

Arusha

Gombe Stream

Katavi

Kilimanjaro

Kitulo Plateau

Mahale Mountains

Lake Manyara

Mikumi

Mkomazi

Ruaha

Rubondo Island

Saadani

Serengeti

Tarangire

Udzungwa

News

9 April 2013

China yahimizwa kuwekeza sekta ya Utalii nchini

Na Pascal Shelutete, Beijing

Tanzania delegation and Chaoyang District Commission of Tourism in Beijing pose in a group picture after their official talks

Tanzania imehimiza wawekezaji kutoka China kuwekeza katika sekta ya utalii ambayo ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumiwa ipasavyo. Mkurugenzi wa Utalii  kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa alisema hayo jana alipokutana na ujumbe Kamisheni ya Utalii ya Chaoyang jijini Beijing  nchini China.

Bw. Mussa ambaye anaongoza ujumbe kutoka Tanzania unaotembelea China kwa lengo la kutangaza utalii wa nchi yetu alisema kuwa Tanzania ina matarajio makubwa ya kupata wawekezaji kutoka China hasa katika maeneo ya uwekezaji wa hoteli ili kuongeza idadi ya vitanda nchini ili kukidhi mahitaji ya watalii wanaofika nchini kutalii. Alisema kuwa utaalamu wa mafunzo kwa ajili ya rasilimali watu katika sekta ya utalii inahitajika ili kuweza kuhudumia watalii wanaofika nchi katika viwango vinavyokubalika kimataifa na hivyo kuwataka Wachina kutumia fursa hizi kuisadia Tanzania.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi alisema kuwa TANAPA imeshaandaa mwongozo kwa wawekezaji unaobainisha fursa mbalimbali za uwekezaji katika Hifadhi za Taifa. Alisema kuwa mwongozo huo hivi sasa umetenga maeneo 25 kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo manne katika Hifadhi ya Serengeti; matatu katika Hifadhi ya Tarangire; sita Hifadhi ya Katavi na manne Hifadhi ya Saadani ambako wawekezaji wanahimizwa kuwekeza ikiwemo kutoka China ambayo ukuaji wake kiuchumi unakwenda kwa kasi kubwa.

Kijazi alisema kuwa hivi sasa wawekezaji katika maeneo ya hifadhi wanatoka katika mataifa ya Marekani na Ulaya na kuwa hakuna wawekezaji kutoka China na kuwahimiza sasa kutumia fursa zilizopo katika hifadhi kwa ajili ya kuwekeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Aloyce Nzuki alihimiza mashirika ya kuratibu safari za wageni yanayomilikiwa na serikali nchini China kufungua matawi ya ofisi zao nchini ili kusaidia kuongeza idadi ya wageni kutoka China kutembelea vivutio vya utalii nchini. Alisema kuwa zipo fursa nzuri za uwekezaji ikiwemo kuanzisha safari za boti katika Ziwa Tanganyika na Victoria pamoja na safari za utalii kwa kutumia usafiri wa treni hasa katika ukanda wa Saadani na Mkomazi.

Pande zote mbili zilikubaliana kubainisha maeneo halisi ya ushirkiano na uwekezaji na kuandaa Hati ya Makubaliano ambayo itawekwa saini na pande zote ikiwa ni njia nojawapo ya kuendeleza uhusiano wa siku nyingi baina ya Tanzania na China ambao uliasisiwa na marais wa kwanza wa nchi hizi hayati  Julius Nyerere na hayati Mao Zedong.

Tanzanian delegation in official talks with officials from Chaoyang District Commission of Tourism in Beijing focusing on promo