NATIONAL PARKS

Arusha

Gombe Stream

Katavi

Kilimanjaro

Kitulo Plateau

Mahale Mountains

Lake Manyara

Mikumi

Mkomazi

Ruaha

Rubondo Island

Saadani

Serengeti

Tarangire

Udzungwa

News

22 May 2013

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII MAIMUNA TARISHI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI NA KUWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi amewataka watumishi wa Hifadhi za Taifa nchini kuzingatia maadili na weledi katika utendaji kazi wao wa kila siku ili kudumisha sekta ya uhifadhi nchini. Bi. Tarishi aliyasema hayo alipokutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wilayani Same, Kilimanjaro hivi karibuni.

Bi. Tarishi alisema kuwa sekta ya uhifadhi nchini inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ile ya ujangili ambayo njia pekee ya kukabiliana nayo ni kuwa na watumishi wenye ari na moyo wa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na uadilifu.

Alibainisha kuwa ujangili unaoendelea dhidi ya rasilimali zinazohifadhiwa unapaswa kupigwa vita kwa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi zote za uhifadhi kupigana vita moja kwa kuwa wanyama wanaowindwa na majangili ni walewale na hawana mipaka katika maeneo mbalimbali yaliyohifadhiwa nchini.

Akizungumzia sekta ya utalii na hasa kufungua eneo la ukanda wa kusini, Bi. Tarishi alisema kuwa eneo hili ni eneo mtambuka kwa maana linahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali na kusema kuwa tayari Serikali imeshaanza kufanyia kazi changamoto ya miundombinu kwa eneo la ukanda wa kusini ili kuvutia wageni wengi zaidi. Alitaja kuwa Uwanja wa Ndege wa Mbeya ni mojawapo ya jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa maeneo ya kusini mwa nchi yetu yanafikika kwa urahisi kwa watalii wanaofika nchini.

Bi. Tarishi ambaye amekuwa katika ziara ndefu ya kutembelea mashirika na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii aliwapongeza watumishi wa Hifadhi ya Mkomazi kwa jitihada kubwa walizofanya katika kusimamia uhifadhi ambapo licha ya hifadhi hiyo kuanzishwa mwaka 2008, tayari mafanikio makubwa yameanza kuonekana ikiwa ni pamoja na uoto wa asili kurudi kwa haraka na hivyo kukaribisha wanyama mbalimbali katika hifadhi hiyo.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mwalimu  Herman Kapufi kujitambulisha.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mwalimu Herman Kapufi kujitambulisha.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa(aliyenyoosha mkono)  akimuonyesha Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi (suti nyeusi) eneo lenye mgogoro wa mpaka katika Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamambaa; Kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa TANAPA Dk. Ezekiel Dembe na Mkurugenzi wa Utumishi Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.

Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi mojawapo ya majengo mapya yaliyojengwa na hifadhi hivi karibuni.

Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi mojawapo ya majengo mapya yaliyojengwa na hifadhi hivi karibuni.

Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alipowatembelea.

Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alipowatembelea.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamamba, Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akipokea kitabu maalum kinachoitwa Born Wild kilichoandikwa na Tony Fitzjohn waMradi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akipokea kitabu maalum kinachoitwa Born Wild kilichoandikwa na Tony Fitzjohn waMradi wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Mkomazi.

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho. .

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho.

Habari na Picha zote na mdau Pascal Shelutete